KIJANA DAUDI BABU MRINDOKO APENDEKEZWA KUWA MLEZI WA UVCCM SHINA LA DOBI KATA YA NJORO,MOSHI MJINI,

Moshi,Kilimanjaro
MCC na Mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Ndg. Sadiffa Juma Khamis(mb), Jumapili 10 Mei 2015 katika mkutano wa hadhara amempendekeza Ndg. Daud Mrindoko kuwa mlezi wa shina hilo na kumtaka awalee vizuri ili ndoto yake ya ubunge itimie. Amesema endapo atatimiza hayo basi yeye kama mjumbe wa kamati kuu atamuunga mkono na pia amewataka wananchi wa jimbo la Moshi mjini kumuunga mkono.
Kijana Daudi Babu Mrindoko alimaarufu kama "Obama wa Moshi" ni kijana ambaye
mwenye mvuto mkubwa na kushawishiwa na wakazi wa jimbo la Moshi mjini achukue fomu ya kugombea ubunge 2015 wa jimbo la Moshi Mjini.Kijana huyo mkazi wa
Moshi mjini anaonekana kukubalika kwa jamii yote wazee na vijana,wanawake na
wanaume,baadhi ya wakazi wa moshi mjini wanamedai kuwa wao awajali chama
gani atagamboe bali wanachotaka ni kumuona kijana huyo analiwakirisha jimbo la Moshi mjini bungeni.wengine wamedai sababu kubwa za kumuunga mkono ni kuwa wanauhakika kuwa Daudi Mrindoko ni mchapa kazi mwenye kuyaelewa mahitaji ya wapiga kura wa Moshi Mjini.