RAIS Pierre Nkurunziza wa Burundi amewahutubia wanahabari mjini Bujumbura ikiwa ni mara ya kwanza tangu arejee nchini humo akitokea Tanzania baada ya jaribio la kutaka kumpindua kukwama.

Rais huyo alirejea Burundi juzi Ijumaa ikiwa ni siku mbili tangu jaribio la kutaka kumpindua kugonga mwamba.