Lowassa_Ilala
Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akiwapungian wananchi wakati akiwasili ofisi za CCM kata ya Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam, kutafuta wadhamini. (Picha na K-VIS MEDIA).
Kingunge udhamini
Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombali Mwiru, (kushoto), akijaza fomu za kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye ofisi za CCM wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 27, 2015, wakati Mh. Lowassa, alipotua jijini Dar es Salaam kutafuta wadhamini. Mh. Lowassa alpata jumla ya wadhamini 212,150, idadi ambayo ni kubwa kuliko mikoa yote ambayo tayari Mh. Lowassa ametembelea hadi sasa.
Kingunge address
Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, akihutubia maelfu ya wana CCM na wananchi wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 27, 2015, wakati Mh. Lowassa, alipofika kutafuta wadhamini mmojawapo akiwa Mzee Kingunge.
Lowassa_tmk
Mh. Lowassa, akitoa hotuba ya kuwashukuru wana CCM wenzake wa wilaya ya Temeke kwenye ofisi za chama hicho wilayani humo Juni 27, 2015.
Ilalashangilia2
Mwana CCM aliyejawa na furaha wakati Mh. Lowassa, aitoa hotuba ya kuwashukuru kwa kumdhamini kwenye ofisi za CCM, kata ya Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam, Juni 27, 2015.
DSC_5122
Mwana CCM aliyejawa na furaha wakati Mh. Lowassa, aitoa hotuba ya kuwashukuru kwa kumdhamini kwenye ofisi za CCM, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 27, 2015.

Kinondoni
Lowassa_walemavu
Mh. Lowassa, akisalimiana na watu wenye ulemavu, waliokuwa miongoni mwa wana CCM na wananchi waliofurika kwenye ofisi za chama hicho kata ya Mchikichini jijini Juni 27, 2015, alipokwenda kutafuta wadhamini.
Polisi airport
Polisi akiwatawanya mamia ya wana CCM na wananchi waliofurika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Juni 27, 2015, wakati Mh. Lowassa akiwasili jijini kuomba wadhamini. 
Lowassa_Pindi Chana
Mh. Lowassa, akisalimiana na Mumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mh. Pindi Chana, walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Juni 27, 2015. Wakati Mh. Lowassa, alikuwa akiwasili jijini akitokea jijini Arusha, Mh. Pindi Chana alikuwa kwenye msafara wa wajumbe wa Kamati Kuu, waliokuwa wakielekea kwenye msiba wa Mbunge wa Geita, Hayati Max.(Picha na K-VIS MEDIA).