Madee-crop 1
Hamad Ally' Madee'
WAFALME kunako Hip Hop na Taarab, Hamad Ally ‘Madee’, Juma Kassim ‘Nature’ pamoja na Mzee Yusuf wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo Idd Mosi hii ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
JUMA
Juma Nature.
Mastaa hao walizungumza na Uwazi Mizengwe kuhusiana na shoo hiyo ambapo kila mmoja aliahidi kufanya makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika tasnia ya muziki huku wengine wakiahidi kuachia nyimbo mpya.

Mja pani Mweusi
Pazia la burudani kwa watoto litafunguliwa na mkali wa sarakasi Bongo anayekubalika nchini Ujerumani na Australia, Ramadhan Adam ‘Mjapani Mweusi’ ambapo Idd Mosi hii atafanya maajabu ya kihistoria.
“Watoto watafurahia tena sana sikukuu hii kwani nitaingia na joka kubwa linaloitwa Anakonda ambapo kila atakayetaka kulishika na kucheza nalo ataruhusiwa kwani halina madhara yoyote. Pia nitakuwa na Dogo Kadogonda ambapo naye ataonesha maajabu ya kujilipua kwa moto na kugaragara huku moto ukimuunguza,” alisema Mjapani Mweusi.
Wakali Dancers.
Wakali Dancers na Masai Warriors
Mbali na Mjapani Mweusi, burudani Idd Mosi hii itawashwa pia na wasanii tishio kwa kucheza na watoto, Wakali Dancers pamoja na Masai Warriors ambapo siku hiyo watawachezesha watoto michezo mbalimbali kwa staili kibao sambamba na mazingaombwe.
“Kila mtoto atakayefika atafurahi na sisi kwani tutamfundisha jinsi ya kucheza muziki kwa staili tofauti na watakaocheza vizuri watapata zawadi kutoka kwa Wakali Dancers,” alisema mmoja wa mastaa wa Kundi la Wakali.
Siku hiyo Dar Live, watoto watacheza michezo ya kuteleza, kubembea, kupanda ndege, mashindano ya kuogelea na motto atakayependeza zaidi ya wenzake atapewa zawadi nono.
Madee
Shoo ya kibabe itaanzia saa moja usiku, ambapo Rais wa Manzese, Madee atatinga na kundi lake la Tip Top Connection kunukisha mwanzo mwisho.
“Mara ya kwanza kupiga shoo Dar Live ilikuwa siku ya uzinduzi wa ukumbi huu miaka kadhaa iliyopita na ilikuwa historia. Idd Mosi hii narudi kwa kishindo nikiwa Madee mpya na ngoma mpya.
Mashabiki watarajie kusikia ngoma zangu zote mpya kama vile Pombe Yangu, Ni Sheeda, Tema Mate Tuwachape na kwa mara ya kwanza nitauzindua wimbo wangu mpya kabisa, mbichiiii ndani ya Dar Live uitwao Kombe,” alisema Madee.
Nature
Mbali ya Rais wa Manzese, rais mwingine kutoka Temeke na mkongwe mwenye miaka zaidi ya 16 kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nature naye atakuwepo sambamba na kundi lake la TMK Wanaume Halisi. “Kama jana, kama juzi, kama kesho, wananiita Kibra ndani ya Dar Live tukutane Idd Mosi hii kwani nitawasha moto wa aina yake.
Sina maneno mengi ila mashabiki wangu wananitambua kwa vitendo kuanzia ngoma zote za zamani hadi sasa ni full kuserereka,” alisema Nature.
MITIKISIKOYAPWANIDARLIVE7
Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf
Ukiachana na wakali wa Hip Hop, usiku huo utasimamiwa pia na kundi linalotikisa Bongo kunako miondoko ya Pwani, Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Mfalme Mzee Yusuf. “Baada ya kukinukisha na tuzo zangu za Kili mwaka huu kwenye shoo ya Vunja Jungu, niwaahidi mashabiki wangu, wapenda Taarab wote waje wamuone mbunge mtarajiwa wa Unguja nikizindua Wimbo wa Kaning’ang’ania Ng’ang’ani na nyingine kibao.
Tutapiga nyimbo zote tisa zilizopo kwenye albamu yetu mpya ya Mahaba Niue kama vile Nina Moyo Sina Jiwe wa Leila Rashid, Siumbuki wa Fatma, Nia Safi Hairogwi wa Mishi na nyingine kibao. Kifupi hatuna maneno mengi bali muziki wetu kila anayetuona jukwaani anajua habari yake inakuwaje,” alisema Mzee Yusuf.
msagasumu2
Msaga Sumu.
Msaga Sumu
Ukiachana na wakali wa Hip Hop na Taarab, mfalme wa nyimbo za Singeli ambaye hana mshindani Bongo, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ naye atakuwepo kuwaburudisha mashabiki wote wa kiswazi na kishua.
“Bila chenga muziki wangu hakuna asiyeujua ni mperampera mwanzo mwisho. Naanza na Historia ya Kweli, Rafiki wa Kweli, Huyo Mtoto, Napenda Simba na nyingine nyingi bila kusahau siku hiyo kwa mara ya kwanza nitatambulisha ngoma yangu mpya niliyoshirikiana na Nature inayoitwa Inaniuma Sana (remix),” alisema Msaga Sumu.
IMG_3875
Pam D.
Pam D
Staa wa Wimbo wa Nimempata anayesumbua vichwa vya mastaa wa muziki wengi wa kike, Pamela Daffa ‘Pam D’ atakuwa miongoni mwa wakali watakaotikisa.
“Ngoma ya Nimempata hakuna asiyeijua, hadi sasa nimepiga shoo kibao ambazo kila mmoja ananipigia saluti. Mashabiki watarajie nikiwa na madensa wangu kuwapa sapraizi za kutosha ikiwa ni pamoja na kuzindua ngoma yangu mpya iitwayo Popolipopo niliomshirikisha Christian Bella,” alisema Pam D.