Mwandishi Wetu
KUFUATIA kuwepo kwa makundi yaliyotokana na watangaza nia 42 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakiwania nafasi ya urais, mastaa waliokuwemo ndani ya makundi hayo wameumbuka kufuatia ushindi wa John Pombe Magufuli, Risasi Mchanganyiko lina ‘full’ stori.
Diamond Platnum.
WAMEUMBUKAJE?
Listi ndefu ya mastaa ikiongozwa na Jacqueline Wolper, Wema Sepetu ‘Madam’, Wastara Juma, Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu, Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Stephen ‘JB’, Bahati Bukuku, Tunda Man, Diamond na wengineo walikuwa wamegawanyika, baadhi wakimuunga mkono Bernard Membe na wengine Edward Lowassa hivyo alipopitishwa Magufuli ambaye hakuwa na wapambe, wakajikuta wameumbuka.
CHANZO CHASHUSHA UBUYU
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mastaa hao, kuumbuka kwao kulikuwa kwa aina mbili. Kuna baadhi walikwenda Dodoma kulipokuwa kukifanyika vikao vya kuwachuja wagombea wakiwa wamejiandaa kwa sherehe lakini kuna ambao walibaki Dar kusikilizia.
“Walikwenda Dodoma wakiwa wameshahakikishiwa ushindi wa Membe na Lowassa, lakini bahati mbaya kwao hakukuwa na yeyote kati yao aliyefanikiwa kupenya, ingawa Membe aliingia Tano Bora,” kilisema chanzo chetu.
Wema Sepetu ‘Madam’.
KIZINGITI KILICHOWAKWAMISHA
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, jina lake halikufanikiwa kuvuka kwenye Kamati Kuu huku Membe ambaye ni Mbunge wa Mtama akiienguliwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu.
WALITINGA DOM KWA MBWEMBWE
Chanzo kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, mastaa hao walitinga Dodoma kwa mbwembwe ikidaiwa kuwa walishahakikishiwa ‘mtonyo’ baada ya mgombea wao kushinda.
“Ilikuwa wameshahakikishiwa ulaji. Wagombea wao waliposhindwa kuvuka, posho zao nazo zikayeyuka papo hapo.”
Kajala Masanja ‘Kay’.
KUMBE WALIANDALIWA SARE
“Yani ishu ilikuwa ni kubwa. Unaambiwa waliandaliwa hadi sare kwa ajili ya kusherehekea ushindi lakini mambo yote yaliharibika baada ya wagombea wao kushindwa,” kilieleza chanzo hicho na kuongeza:
“Yaani waliumbuka kwelikweli maana kuna ambao hawakwenda Dodoma lakini walikuwa wamewakilishwa na wenzao walioenda na mikakati yao ilikuwa wangepita wagombea wao, wangeungana kuwapigia kampeni nchi nzima.
Vicent Kigosi ‘Ray’
WASIOKWENDA DODOMA
Risasi Mchanganyiko limechimba wasanii ambao wanadaiwa kutokwenda Dodoma na kutajwa kuwa wamewakilishwa na wenzao huku wakipiga kampeni kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni pamoja na Jacqueline, Wema, Lulu, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Bahati Bukuku na Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
WALIOENDA DODOMA NI KINA NANI?
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, miongoni mwa wasanii waliokwenda Dodoma na kudaiwa kujipanga kwa sherehe hizo za ushindi wa makundi ya wagombea ni pamoja na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, JB, Kajala, Ray na Wastara.
STEVE NYERERE AFUNGUKA
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya Steve Nyerere ambaye alikanusha kuwepo kwa sherehe iliyopangwa lakini aliungana na wenzake waliokwenda kumuunga mkono Membe lakini kwa kuwa hakushinda, wamehamia kwa Magufuli.
“Sisi hatukuandaliwa sherehe, mimi JB, Kajala, Ray na Wastara tulikwenda kumuunga mkono Membe na tulipewa chetu, sasa kwa kuwa mgombea wetu ameshindwa tulihamia kwa Magufuli ambaye ni timu moja na Membe,” alisema Steve.
0 Comments