sdfDk. Joseph Chilongani aliyepigwa akiwa amezimia.
Job NdugaiJob Ndugai.
Mbunge wa Kongwa kwa tiketi ya CCM aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amempiga mgombea mwenzie wa nafasi ya ubunge, Dk. Joseph Chilongani kwa madai ya kumpiga picha wakati anafanya fujo kwenye mkutano wa kampeni wa kura za maoni.

Tukio hilo limetokea jana jioni wakati wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM wakiwa kwenye Mkutano na wao kwa ajili ya kujinadi kwenye kata ya Ugogoni iliyopo wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mdogo wa Dk. Chilongani, Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya mmoja wa wagombea anayejulikana kama Simon Ngatunga kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kuahidi kuwa kama atakuwa mbunge atahakikisha kuwa anaziba mianya yote ya ubadhirifu na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini kauli iliyomkera Job Ndugai. Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..
Ilipofika zamu ya Ndugai kujinadi kwa wanachama wa CCM alimtuhumu Ngatunga kwa kusema uongo na kwamba hakuna ubadhirifu wa aina yoyote ndani ya Halmashauri hiyo.
Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.
Amesema Ndugai aliposhuka jukwaani alianza kumtafuta Ngatunga ili ampige kwa fimbo ambayo huwa anatembea nayo kwenye kampeni hizo.
Wakati akifanya fujo za kumpiga mgombea huyo, Dk. Chilongani alikuwa anampiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi ambapo Ndugai alipomwona alianza kumshambulia kwa fimbo katika maeneo ya tumboni na kichwani hali iliyomfanya mgombea huyo kupoteza fahamu papo hapo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa hana taarifa kuhusiana na tukio hilo ambapo Job Ndugai simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.
Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.
Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..