Nahodha na golikipa wa Liege Sele Rasta akilinyanyua kombe juu kwa furaha huku wachezaji wenzake wakimsaidia kushangilia ushindi wao dhidi ya timu ya Antwerpen Fc hapo jana katika uwanja wa Leuven.

Mabingwa wa mashindano ya Bonanza kwa mwaka 2015 timu ya Liege ikishangilia ushindi wao wa kulinyakua kombe dhidi ya timu pinzani ya Antwerpen baada ya kuifunga kwa penati 4 -2

Kikosi cha timu ya Liege ambacho ni mambingwa kwa msimu huu wa mwaka 2015-2016 

Mshambuliaji wa timu ya Liege Ronda Rasta akiukokota mpira baada ya kuitoka ngome ya timu ya Antwerpen katika mchezo mkali wa jana ambao ulichezwa katika kiwanja cha cha jiji la Leuven,mpaka mwisho wa mpira timu ya Liege ilitoka kinara baada ya kulitwaa kombe

Hekaheka katika lango la timu ya Antwerpen huku mabeki wa timu hiyo wakijitahidi kuokoa hatari langoni mwao

Jitihada za golikipa Sele Rasta wa Antwerpen hazikufua dafu baada ya kushindwa kuokokoa mkwaju mkali uliopigwa na Issa na  kwenda moja kwa moja wavuni 

Wazee wa kazi wakiendelea kupongezana kwa timu zao zinavyofanya vyema uwanjani

Nyambi kulia akisikitika kwa uchungu baada ya kuona timu yake ya Antwerpen inapachikwa bao la kwanza dhidi ya Liege


Kwenye benchi la ufundi ni ndugu Joseph anayenyoosha mkono kutoa maelekezo kwa timu yake ya Anwerpen wakati wa mapumziko

Kikosi cha Antwerpen Fc ambacho kiukweli kilileta changamoto kubwa sana katika mashindano haya ya msimu huu wa Bonanza la mwaka 2015

Kikosi cha Liege ambacho kilichanganyika na baadhi ya wachezaji wa Antwerpen kwa picha ya kumbukumbu

Baadhi ya wachezaji wakali wa timu ya Antwerpen

Benchi la ufundi likiongozwa na kaka yetu mtaalamu Mchawi wa wachawi

Hiki ndicho kikombe walichotwaa wana wa Liege

Baada ya mpira kuisha waandaji wa mashindano haya walitoa shukrani za pongezi kwa vilabu vyote vilivyoshiriki kwa nidhamu walizozionesha,upendo na burudani kwa mchezo wao,waandani walitoa zawadi kwa golikipa bora wa mashindano na mchezaji bora wa mshindano

Golikipa bora wa mshindano hayo Qwiyala wa timu ya Antwerpen akipokea kikombe kutoka kwa mmoja wa wageni waalikwa

Mchezaji bora wa Mashindano kutoka timu ya Antwerpen akipokea zawadi yake kutoka kwa mgeni mualikwa.Picha na maelezo zaidi yatafuata hapo baadae.