Image copyrightno credit
Image captionRais Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani Barack Obama imehudhuria hafla ya kumbukumbu uharibifu katika mji wa New Orleans uliosababishwa na kimbunga Katrina miaka kumi iliyopita.
Katika hotuba yake kile kilichoanza kama maafa ya asilli yamekuwa maafa yaliyotengenezwa na binadamu ambapo serikali ilishindindwa kuwaangalia raia wake.

Obama anatarajiwa pia kuonyesha kukosekana kwa miundombinu imara ya mji wa New Orleans kwa wakati huo.
Nyumba nyingi zilizokumbwa na mafuriko kwa wakati huo zilikua za udongo mwepesi na ni vitongoji vya watu weusi maskini kwenye mji huo.
Zaidi ya watu elfu moja na mia nane walifariki katika maafa hayo ambayo ni mabaya kutokea tangu mwaka 1928 na (kusababisha uharibifu mkubwa katika pwani ya Ghuba kutoka Florida na Texas. )