Image copyrightBBC World Service
Image captionWahamiaji wakisafiri katika pwani ya Libya
Zaidi ya watu mia mbili wanahofiwa kufariki baada ya boti mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu kuzama katika eneo la Zurawa pwani ya Libya.
Mamia ya wahamiaji wengine wameokolewa na wanamaji wa Libya usiku wa kuamkia leo.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja Libya haijakuwa na serikali dhabiti na sehemu kubwa ya nchi hiyo inathibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu, na walanguzi wa watu wanatumia fursa hiyo kusafirisha watu kimagendo hadi Ulaya.

Kwa mara ya kwanza wakaazi wa mji huo waliandamana kupinga usafirishaji wa watu kupitia mji huo.
Ripoti zinasema kuwa meli mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji hao zilizama muda mfupi tu baada ya kunoa nanga.
Meli moja inasemekana kuzana usiku wa kuamia siku ya Alhamisi na nyingine saa chache baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa shirika la uhamiaji la kimataifa IOM, nchini Libya, watu mia moja tayari wameokolewa na kusafirisha hadi kambi moja ya muda iliyoko mji wa Sabratha.
Amesema wengi wa manusura hao ni wanaume lakini wamefanikiwa kuwaokoa wanawake tisa na watoto wawili.
Vyanzo vya habari mjini Zuwara zinasema kuwa miili ya watu mia moja zimehifadhiwa katika hospitali moja mjini humo.
Walioangamia kwenye ajali hiyo ni raia wa Syria, Bangladesh na mataifa kadhaa ya Afrika.