TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema majina ya wabunge wa Viti Maalumu iliyoyapitisha hayajachakachuliwa bali yamepitishwa kulingana na orodha ya vyama vya siasa vilivyowasilisha majina hayo.
Kauli hiyo imetokana na kuwepo kwa taarifa ya malalamiko kutoka katika baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikidai kuchakachuliwa kwa majina waliyoyawasilisha katika tume hiyo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima alikanusha taarifa hizo Dar es Salaam jana wakati akitangaza majina ya Madiwani wa Viti Maalumu wa vyama vya siasa katika kata zote nchini. Kailima alisema, orodha iliyotumiwa na tume ni ile ambayo iliwasilishwa na vyama vya siasa ambapo orodha ya tume ilifuata kama vyama hivyo vilivyokuwa vimeorodhesha.
“Majina ya wabunge wa Viti Maalumu hatujayachakachua, tulitumia majina tuliyoletewa na vyama vya siasa kwa kuzingatia sifa,” Kailima alisema. Kumekuwa na madai ya ukiukwaji wa uteuzi wa majina ya wabunge hao wa Viti Maalumu kwa baadhi ya vyama vikiwamo Chadema na Chama Cha Mapinduzi ambavyo baadhi ya wanachama wake wamelalamikia uteuzi huo.
Akitangaza majina ya madiwani hao, Kailima alisema CCM imepata madiwani 1,022, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) 280, ACT-Wazalendo madiwani sita na NCCR-Mageuzi kimepata madiwani sita.
Alisema, idadi ya viti hiyo inatokana na ya madiwani wa kuchaguliwa 3957 wa kata zote nchini, ambapo vimebaki viti 15 ambavyo vinasubiri kukamilika kwa chaguzi ndogo ambazo zitamalizika Desemba 20, mwaka huu.
Aidha, Kailima alisema katika baadhi ya kata baadhi ya vyama vya siasa havijawasilisha majina ya madiwani wake ambao wanatakiwa kupitishwa na NEC kama wana vigezo. Alisema wametangaza majina hayo ili kuepusha kuonekana kuwa tume imechelewesha kutoa majina hayo, kwa sababu sheria inaelekeza kuwa mabaraza ya Halmashauri yaundwe siku 30 baada ya kufanyika uchaguzi.
Akizungumzia uchaguzi katika majimbo ambayo yaliahirishwa katika maeneo mbalimbali nchini, Kailima alisema Novemba 22, mwaka huu uchaguzi utafanyika katika majimbo ya Lushoto na Ulanga Mashariki ambayo uchaguzi uliahirishwa kutokana na vifo vya wagombea. N
|
0 Comments