Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Watuhumiwa hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum (sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa haowalikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia. |
0 Comments