Mkuu wa huduma ya magereza katika mji Buenos Aires Argentina amefutwa kazi baada ya wafungwa watatu mashuhuri kutoroka kutoka gereza lenye ulinzi mkali siku ya Jumapili.
Gavana wa jimbo hilo , Bi Maria Eugenia Vidal , alisema yeye alichukua hatua hiyo kwa sababu kulikuwa na ushahidi kwamba wafungwa wote walisaidiwa na maafisa wa idara ya magereza kutoroka .

Image copyrightPA
Image captionYamkini walitoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi wakitumia bunduki bandia
Wafungwa hao Victor Schillaci na kaka wawili Cristian na Martin Lanatta, walikuwa wanatumikia hukumu ya maisha gerezani kwa makosa ya utekaji nyara na mauaji ya wafanyabiashara watatu katika tukio lililohusishwa na mzozo wa madawa ya kulevya mnamo mwaka wa 2008.
Yamkini walitoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi wakitumia bunduki bandia kutishia moja wa walinzi.