manchester-united-vs-chelsea-850x560
Ligi Kuu ya Wingereza jana usiku imeendelea kwa kuchezwa michezo nane katika viwanja tofauti huku mchezo mkubwa uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni kati ya Manchester United na Chelsea mchezo uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford.
Mchezo huo ulisubiriwa na wengi kutokana na hali zilizonazo timu hizo kwa sasa hivyo kuifanya dunia kusubiri mchezo huo kuona nani ataweza kumshinda mwenzake lakini mchezo huo ukaishia kwa sare ya bila kufungana.

Manchester United kama kawaida yao walimiliki mpira kwa muda mwingi wa mchezo huo lakini ikawa na shida katika kumalizia pasi za mwisho huku Chelsea wakionekana kucheza kwa tahadhari wakimwacha mbele Eden Hazard ambaye alionekana kuwa na usumbufu katika eneo la Manchester United.
Timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu lakini hadi dakika 90 zinamalizika hakuna aliyefanikiwa kuingia katika nyavu za mwenzake.
Matokeo mengine ya michezo ya jana;
Manchester United 0 – 0 Chelsea
Crystal Palace 0 – 0 Swansea
Everton 3 – 4 Stoke City
Norwich 2 – 0 Aston Villa
Watford 1 – 2 Tottenham Hotspur
West Bromwich Albion 1 – 0 Newcastle United
Arsenal 2 – 0 AFC Bournemouth
West Ham United 2 – 1 Southampton