Familia ya Bw. Mgalula Fundikira inasikitika kuwataarifu ndugu, jamaa na marafiki kuwa mwanawe Mlawila (Lawi) Fundikira (18) (pichani) amefariki dunia alfajiri ya Jumamosi  katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kulazwa kutokana na ajali ya gari aliyopata alfajiri ya Jumapili ya tarehe 12/11/2015.

Msiba upo Kinondoni block 42 (Bwawani) mtaa ilipo Facebook take away. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni katikai makaburi ya Kisutu. 

Mwili wa marehemu ukiondolewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili muda huu kuelekea nyumbani Kinondoni kwa maandalizi kabla ya Mazishi.