Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa asubuhi hii ili Wananchi wa Rwanda zaidi ya milioni sita leo wapige kura ya maoni kukubali ama kukataa kubadili katiba ili kumruhusu Rais wa nchi hiyo Paul Kagame kugombea tena kiti cha urais.
Lengo la kura hiyo ya maoni ni kumwongezea rais wa nchi hiyo Paul Kagame muhula mwingine wa utawala.
Kama vifungu hivyo vitapitishwa itatoa fursa kwa Rais Kagame kuweza kukaa madarakani hadi mwaka 2034.
Hatua hiyo imepingwa vikali na Marekani na Umoja wa nchi za ulaya pamoja na baadhi ya wanaharakati na vyama vya upinzani.
|
0 Comments