Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na watendaji wengine serikalini, kutumia vizuri fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, na kwamba wote watakaobainika kutumia fedha hizo vibaya watashughulikiwa mara moja, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa michezo wa Ilulu mkoani Lindi, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu
ateuliwe kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya 5 baada ya uchaguzi mkuu, ziara itakayomfikisha kwenye jimbo lake la uchaguzi la ruangwa, waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema pamoja na serikali kuwachukulia hatua kali, ikiwemo kuwafukuza kazi wakurugenzi wa watendaji wengine wa serikali, watakaotumia vibaya fedha za miradi ya maendeleo, amewataka wakurugenzi wenye moyo wa kuwatumukia wananchi wasihofu, kwa kuwa serikali ipo pamoja nao.
Aidha amesema serikali ya awamu ya 5 haina ugomvi na wafanyabiashara kama baadhi ya watu wachache wanaojaribu kuchonganisha, na badala yake serikali itaendelea kujenga mahusiano mazuri nao katika kuhakikisha wanalipa kodi halali, na kusisitiza, yeye kama waziri mkuu atalisimamia kwa nguvu zote jambo hilo.
Kwa upande wake, mheshimiwa Nape Nauye akizungumza kama katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, amewataka wanaccm kote nchi kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya 5 ya kuhimiza uwajibikaji na kufichua wezi wa mali za uma.