Mshambuliaji machachari wa Manchester United,Wayne Rooney akiifungia  timu yake ya Manchester bao muhimu katika dakika ya 78 ya mchezo kati yao na Liverpool.Mchezo ambao umechezwa leo katika uwanja wa Anfield na mpaka mwisho wa mchezo Manchester United imeibuka mshindi wa bao hilo 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Liverpool.

Wachezaji wa timu ya Manchester wakishangilia ushindi wao wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool uliochezwa leo katika uwanja wa Anfield nchini Uingereza.