•             Ni mtandao wa kasi Zaidi
na wenye uwigo mpana Tanzania

 Kampuni ya simu za mkononi ya
Tigo ambayo inaongoza kwa kuendesha maisha ya kidijitali imetangaza mpango wake
wa kupanua huduma ya intaneti ya 4G katika mikoa yote nchini mwaka huu.

 Huduma hiyo ilizinduliwa jijini Dar es
Salaam  mwanzoni mwa mwaka jana  na
baadaye ilisambazwa kwenye mikoa ya Arusha, Tanga, Dodoma na Morogoro,
kwa ufanisi na  hivyo kuufanya mtandao wa
4G kuwa mpana na wa kasi nchini Tanzania.

 Ukichukuliwa kama teknolojia nzuri ya hivi
karibuni kwenye sekta ya mawasiliano duniani isiyo na dosari katika kuifikia
huduma ya intaneti, teknolojia ya 4G LTE ina kasi ya nguvu takribani mara tano
ikilinganishwa na teknolojia ya 3G ambayo inatumiwa na watoaji wengine wa
huduma hiyo kwenye soko la Tanzania.


Mtandao wa 4GLTE una kasi
kubwa kwenye kurambaza (surf) na kupakua vitu mbalimbali  kutoka kwenye intaneti pamoja na kupiga miito
ya simu ya skype.
Hali kadhalika  inawezesha wateja kwa kiwango kikubwa  kuwa na uzoefu wa kutiririsha video au
kufanya mikutano na inaweza kuhimili
kutumika kwenye  kupata video,
mikutano, muonekano wa hali ya juu, blogu za video, michezo mbalimbali  na kupakua video kwenye mitandao ya kijamii.

Ofisa Biashara Mkuu wa Tigo Shavkat Berdiev


Ofisa Biashara Mkuu wa
Tigo Shavkat Berdiev alisema kwenye taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya
habari  kuwa  mipango ya kupanua teknolojia ya 4G hadi
kwenye maeneo yote nchini  inafanyika
ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo  ya
kuwapatia wateja wake huduma ya hali ya juu duniani ili kuwawezeshakuendesha maisha
ya kidijitali.
“Upanuzi wa
mtandao  wa 4G nchi nzima  kwa mara nyingine umeonesha  sio tu kwamba Tigo  inaongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa
na ya hali ya juu pamoja na ubunifu kwenye soko, bali pia kujikita kwake  kuongeza kufikiwa kwa intaneti kwa Watanzania
wengi kadri iwezekanavyo,” alisema Berdiev.

 Tangu mwaka jana Tigo ilishawekeza dola
milioni 120 kwa mwaka kwenye  upanuzi wa
mtandao wake pamoja na kuboresha maeneo ya mitandao ya 4G na 3G na mkongo wa
mawasiliano. Hali kadhalika kuongeza A
idadi ya kufikiwa kwa huduma kwa wateja nchi nzima.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) takribaniu asilimia 67  ya idadi ya watu wazima wanamiliki simu za
mkononi  ambapo idadi ya watumiaji wa
intaneti hadi mwaka 2014 ilikuwa imeongezeka hadi kufikia watu milioni 9.3.