Wizara ya Mambo ya nje ya Uingereza imesema inachunguza picha ya video iliyosambazwa na Wapiganaji wa Islamic State inayoonyesha wanaume watano wanaodhaniwa ni raia wa Uingereza wakiuawa kwa kupigwa risasi kwa madai ya kufanya ujasusi.
Katika picha hiyo ya video mtu mmoja anayezungumza lafudhi ya Kiingereza anaonekana akitoa tishio kwa nchi ya Uingereza.

Pia video hiyo imemwonyesha kijana mdogo anayezungumza kiingereza pia akizungumzia kuwaua waisioamini.
Kundi la wapiganaji hao wa IS wametoa video hiyo inayoonyesha mtu aliyejifunika uso akiongea kwa lafudhi ya kiingereza akitishia Uingereza kuhusu hatua yake ya kijeshi dhidi ya wapiginaji hao nchini Iraq na Syria.
Video hiyo ya dakika kumi iliyotengenezwa na kundi linaloitwa AL Raqqah na kurushwa kupitia chaneli kuu ya IS inaonyesha mauaji ya watu watano wanaokiri makosa yao.Watu hao watano walionekana kwenye jangwa wakipigwa risasi baada ya kutoa tamko kuwa wanakiri kuwa wamekosa.
Mmoja kati wanaume hao waliouawa anadaiwa kuwa alitumwa kupeleleza taarifa za mahali walipo wapiganaji wa IS, wakiwemo waingereza wawili ili kusaidia kuwashambulia ikiwa ni pamoja na kuwasmbulia kwa njia ya anga.
Wanaume wengine ambao nao walipigwa risasi wanaelezwa kuwa wamekuwa wakiendesha biashara ya duka la mtandao wa internet katika eneo la Al Raqqah na walikuwa wamepewa jukumu la kufanya upelelezi dhidi ya wapiganaji hao wa IS wanaofika katika biashara yao.
Kijana huyo muaji aliyefunika uso wake anaonekana akimkebehi Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon kwa kupinga nguvu ya IS kabla ya kutoa vitisho kwa Uingereza kuwavamia na kushambulia wapiganaji hao kijeshi.
Kabla ya kuwapiga risasi kichwani kijana huyo mkatili amewajumuisha wanaume hao kuwa walikuwa wapelezi kutoka serikali ya Uingereza.
Video hiyo imehitimishwa ambapo kijana mdogo anaonekana akizungumzia kwa lugha ya kiingereza kuhusu kuuawa kwa watu wasioamini.