Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi hicho pembeni yake ni  Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam"
Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu mafanikio ya kipindi hicho   katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.
Mwandishi wa habari kutoka kituo cha Luninga EATV David Gumbo akiuliza swali kwa mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto mapema leo  kuhusu mafanikio ya kipindi hicho   katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.

Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa akijibu maswali kutoka kwa   waandishi wa habari  kuhusu mafanikio ya kipindi hicho Katikati ni  Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro na kulia kwake ni Mshauri Nasaha Mwandamizi kutoka CSEMA Fatuma Kauramba  katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.


Waandishi wa habari wakisikiliza makini maelezo ya waaandaji  wa kipindi cha Walinde Watoto mapema leo  katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam.






Na Krantz Mwantepele, Dar es salaam

Kuhusu
Kipindi cha Walinde Watoto
Ndugu waandishi wa habari,
katika jitihada za kutoa elimu kuhusu maswala ya Ukatili dhidi ya Watoto,
UNICEF na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa
ushirikiano na True vision production, walianzisha
kipindi cha redio cha Walinde Watoto, ambacho kilianza kuruka hewani kupitia
redio mbalimbali hapa nchini mwezi Novemba mwaka 2014. Kipindi hiki kinarushwa
na redio 19 nchini Tanzania, bara na visiwani, zikiwemo TBC na ZBC.

Malengo
ya Kipindi

Malengo ya Kipindi

Ndugu waandishi wa habari, kipindi cha redio cha Walinde Watoto kilianzishwa kwa malengo yafuatayo;



  1. Kutoa elimu juu ya ulinzi kwa watoto, kufuatia ripoti iliyotolewa mwaka 2011 ambayo ilionyesha ukatili dhidi ya watoto ni tatizo kubwa nchini Tanzania
  2. Kutoa fursa kwa jamii kujadili mazingira salama ambayo mtoto anapaswa kuishi mahali popote atakapokuwa iwe ni nyumbani, shuleni na hata barabarani
  3. Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu na  mbinu za kuripoti matukio ya ukatili kwa watoto.
Mafanikio
ya Kipindi
Ndugu waandishi wa habari,
tangu tumeanza kurusha kipindi cha Walinde Watoto tunajivunia mafanikio mengi;

  • Kwanza kabisa ni kwa
    vituo vya redio vipatavyo 19 kukubali kushiriki kampeni hii kwa kurusha
    kipindi cha elimu kwa umma bila malipo. Tulianza na redio 14 zikiwemo TBC
    na ZBC na miezi michache baadaye ziliongezeka redio nyingine 5 baada ya
    kuvutiwa na maudhui ya kipindi.
    Kwa ujumla kipindi cha Walinde Watoto kinasikika
    nchi nzima.

  • Tumefanikiwa pia
    kutembelea wilaya zaidi ya 12 nchini Tanzania ili kuhakikisha kwamba
    tunatoa fursa kwa watu mbalimbali wakiwemo wazazi na walezi kupaza sauti
    zao katika mambo yahusuyo ulinzi kwa watoto. Miongoni mwa wilaya
    tulizotembelea ni pamoja na Shinyanga, Magu, Musoma, Geita, Kasulu na
    Kahama. Nyingine ni Kilosa, Kigoma, Kasulu, Kisarawe, Hai na zile za
    Zanzibar.

  • Ndugu waandishi wa
    habari tumefanikiwa kutengeneza na kurusha vipindi zaidi ya 60 vikiwemo
    vipindi maalum kuhusu mada mbalimbali kama vile ukatili wa aina mbalimbali wanaofanyiwa watoto wakikiwa nyumbani,
    shuleni, na hata barabarani wakienda na kutoka shule, watoto ulemavu wa ngozi ama albino
    pamoja na watoto wakimbizi. Tumetoa elimu umuhimu wa kutoa taarifa katika
    ngazi tofauti pamoja na namba maalum ya msaada wa watoto ya 116.


  • Ndugu waandishi wa
    habari, jukumu la kuwalinda watoto ni letu sote. Kwa kutambua hili
    tumefanikiwa kufanya mahojiano na viongozi mbalimbali wa serikali,
    viongozi wa dini, viongozi wa taasisi na mashirika binafsi,
    wafanyabiashara, wadau mbalimbali, wanaharakati n.k yote ikiwa na lengo la
    kupata mitazamo tofauti ya wadau hawa muhimu katika maendeleo ya taifa
    letu.

  • Ndugu waandishi wa
    habari, wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tulifanikiwa kufanya
    vipindi maalum vinavyohusu uchaguzi, tuliandaa midahalo iliyowaleta pamoja
    wananchi na watoto katika meza moja na wagombea wao wa ngazi za ubunge na
    udiwani, ili wasikilize ajenda za watoto katika uchaguzi mkuu na kuwaeleza
    ni kwa namna gani wamejipanga kukabiliana na changamoto zinazohusu ulinzi
    wa watoto.

  • Kama mnavyofahamu
    swala la kubadili tabia linahitaji nguvu zetu wote na ni mchakato wa muda
    mrefu, kwa upande wetu, kupitia kipindi hiki cha redio, kwa asilimia kubwa
    tumefanikiwa kuongeza uelewa wa jamii kuhusu maswala yahusuyo ukatili kwa
    watoto na namna mbalimbali za kuwalinda watoto. Tunatumaini mtatuunga
    mkono katika jitihada hizi.

  • Ndugu waandishi wa
    habari, tulifanikiwa kufungua tovuti maalumu ya www.walindewatoto.org
    ambayo imekuwa ikirusha vipindi hivi vya watoto. Tumeweza kufungua akaunti
    katika mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, Twitter na Whatasapp na kwa
    kupitia mitandao hiyo tumeweza kufikia maelfu ya watu. Pia tumeanzisha
    namba maalum ya simu ambayo watu wanaweza kupiga na kutoa maoni yao kuhusu
    vipindi.

  • Ndugu waandishi wa
    habari, kwa kutambua mchango wa redio katika kupiga vita ukatili dhidi ya
    watoto, mnamo mwezi Februari mwaka 2015 tuliweza kutoa mafunzo kwa
    waandishi wa habari kutoka redio zote washirika wa kipindi hiki. Mafunzo
    hayo yaliweza kuwajengea uwezo ili waweze kuzungumzia ukatili kwa watoto,
    namna mbalimbali ya kuwahoji watu ili kuibua changamoto za watoto, na
    namna ya kufanya jamii ibadilike na kuona matatizo ya watoto ni yetu sote.

  • Kutokana na ubora wa
    kipindi, wasikilizaji wengi wameongezeka kitendo ambacho kimewashawishi
    wamiliki wa vituo binafsi kuongeza muda wa kipindi kutoka nusu saa hadi
    saa nzima na hivyo kupokea maswali na mijadala yahusuyo watoto kutoka
    katika maeneo yao.

  • Tumefanikiwa pia
    kuanzisha vikundi vya wasikilizaji kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao
    husikiliza kipindi kila kinaporushwa na kisha kutupa mrejesho wa yale
    waliyojifunza. Makundi haya husambaza elimu waliyoipata kwa watu wengine
    wakiwemo ndugu na marafiki zao.


Tunafanyaje kazi?
Kipindi cha Walinde Watoto
kinapata maudhui (content??) kwa kuandaa midahalo mbalimbali, mikutano katika
vijiji, mahojiano na wadau, kutembelea wilaya na mikoa mbalimbali pamoja na
kupitia mitandao ya kijamii.

Tangu tumeanza kurusha
kipindi, tumeandaa nyimbo mbili maalum kwa ajili ya kampeni.
Kama motisha kwa
wasikilizaji wetu, tunaandaa mashindano mbalimbali ambapo washindi hupata
zawadi mfano fulana (Tshirts), redio n.k

Nini malengo yetu?
Ndugu waandishi wa habari,
mwezi wa kwanza mwaka huu tumeanza msimu wa pili wa kipindi cha Walinde Watoto.
Tunakusudia kufanya yafuatayo;

  • Kushawishi redio
    mbalimbali nchini zishiriki kampeni na kurusha kipindi cha elimu kwa umma.
    Tunakusudia kuongeza idadi ya redio kufikia walau 25 ili tuweze kufikia
    wasikilizaji takribani milioni 24 nchini Tanzania.

  • Kama tunavyofahamu,
    maswala ya ukatili kwa watoto yanazidi kushika hatamu. Awamu hii itajikita
    zaidi kwenye kuzungumzia adhabu mbalimbali za watoto zikiwemo vipigo,
    matusi, manyanyaso, ukatili wa kisaikolojia na nyingine nyingi.

  • Tunakusudia kutumia
    namba maalum ya simu kutoka UNICEF kufanya utafiti kuhusu usikilizaji wa
    kipindi hiki ili kupata mrejesho kutoka kwa wasikilizaji

  • Kuendeleza na
    kuyajengea uwezo makundi ya wasikilizaji wa kipindi katika jamii
    ‘community listening groups’

  • Kuongeza nguvu katika
    matumizi ya mitandao ya kijamii ili kufikia watu wengi zaidi pamoja na
    kutembelea Wilaya nyingine nyingi.
Wito
  • Tunatoa wito kwa
    serikali na taasisi mbalimbali kuendelea kutoa ushirikiano ili tuweze
    kuwahabarisha na kuwafikia watanzania wengi zaidi katika kuhamasisha
    kuwalinda watoto.

  • Tunatoa wito kwa
    wazazi na walezi kuendelea kuwajali na kuwalinda watoto wao kama njia
    mojawapo ya kutimiza majukumu yao kama wazazi.

  • Pia tunatoa wito kwa
    watanzania kwa ujumla kushirikiana kwa karibu na kamati za ulinzi na
    usalama wa mtoto katika kulisukuma gurudumu hili la ulinzi na usalama kwa
    mtoto

  • Endapo utaona mtoto
    anafanyiwa kitendo cha ukatili basi usisite kupiga namba 116 kwa msaada
    zaidi, namba hii ni bure kabisa.

Redio zinazorusha kipindi
cha Walinde Watoto
Zifuatazo ni redio zinazoshirikiana
nasi katika kurusha kipindi cha Walinde Watoto:
1.     Radio
Faraja- Shinyanga
2.     Radio
Huruma- Tanga
3.     Country
FM –Iringa
4.     Ice FM-
Makambako
5.     Radio
Boma Hai- Hai
6.
    Zenji FM –Zanzibar
7.
    Bomba FM –Zanzibar
8.
    Radio Maria- Dar Es Salaam
9.
    Radio Quran- Dar Es Salaam
10.  Best FM – Ludewa
11.  Radio Victoria –Musoma
12.  Dodoma FM – Dodoma
13.  Zanzibar Broadcasting
Cooperation ZBC- Zanzibar
14.  TBC
Taifa- Dar Es Salaam
15.  Radio
FADECO- Karagwe
16.  Radio
Jamii Kilosa- Kilosa
17.  Radio
Kwizera- Ngara
18.  Radio Upland- Njombe
19.  Radio Kitulo- Makete.
Mwisho
Ndugu waandishi wa habari
narudia tena kusisitiza, jukumu la kuwalinda watoto ni jukumu letu sote. Vyombo
vya habari tuna nafasi kubwa sana ya kufikia watu wengi zaidi, tutumie taaluma
yetu kutetea na kulinda haki za watoto.
Asanteni sana kwa
kunisikiliza.