M'mishenari mmoja wa zamani kutoka nchini Marekani amehukumiwa miaka 40 jela kwa kuwanyanyasa kingono watoto mayatima katika nyumba moja nchini Kenya.
Matthew Lane Durham mwenye umri wa miaka 21,alitekeleza ''kitendo hicho kiovu kwa watoto wasioweza kujitetea'',mahakama ya Marekani ilisema.
Durham aliwalenga watoto mayatima alipokuwa kifanya kazi ya kujitolea katika nyumba ya mayatima ya Upendo Childrens Home katika mji mkuu wa Kenya Nairobi,kati ya Aprili na mwezi Juni 2014.
Ni mfanyikazi wa hivi karibuni wa shirika la wahisani kushtakiwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.
Mwaka uliopita,mkuu wa shirika moja la hisani Simon Harris mwenye umri wa miaka 55 alihukumiwa kifungo cha miaka 17 jela na mahakama ya Uingereza kwa kuwanyanyasa watoto wa kurandaranda mitaani kati ya mwaka 1996 na 2013 katika mji wa kilimo wa Gilgil katika mkoa wa Bonde la ufa.
Mwanzilishi wa nyumba ya Upendo ,Eunice Menja alilia alipokuwa akisoma taarifa katika mahakama mjini Oklahoma,akisema kuwa unyanyasaji wa kingono uliofanywa na Durham haukuwa usaliti wa lengo la nyumba hiyo bali pia uaminifu wa Upando kwake, AP iliripoti.
''Matthew Durham aliwabaka watoto.Matthew hana huruma.Alipopatikana bado alikana kutekeleza kitendo hicho,'' alinukuliwa akisema.
Ijapokuwa Durham aliyakana mashtaka hayo,aliongezea kwamba mashtaka dhidi yake yameharibu sifa za nyumba hiyo ya Mayatima.
''Watoto wa Upendo hawastahili kitu kama hiki,''Durham alisema.
Mahakama pia iliagiza kwamba Durham alipe dola 15,863.
|
0 Comments