1Jokate akisaini kitabu cha wageni hospitalini hapo.
2Akitoa zawadi kwa mama aliyejifungua watoto mapacha.
3Jokate (kushoto)akiwa amempakata mtoto mchanga.
4Jokate (aliyeshika maua) akiwa na kruu yake, chini ni maboksi ya zawadi alizopeleka hospitalini hapo.
5Mganga Mkuu wa Palestina, Dk. Kariamel Wandi (mwenye shati jeusi) akitoa shukrani kwa Jokate mbele ya waandishi wa habari.

Ikiwa leo ni Siku ya Wanawake Duniani, mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo amesherehekea na kinamama wajawazito na waliojifungua katika Hospitali ya Palestina Sinza, Dar kwa kuwapa zawadi mbalimbali.
Akizungumza hospitalini hapo, Jokate alisema ameamua kusherehekea na wanawake hao kwa kuwapa zawadi mbalimbali kama vile viatu, dawa za meno kutoka kwenye kampuni yake ya Kidoti kwa sababu leo ni siku muhimu sana kwa wanawake wote duniani hivyo akaona siyo vyema kusherehekea peke yake.
“Nina furaha sana kwa siku ya leo kwani ni muhimu kwetu sisi wanawake, nimeamua kugawana kidogo ninachopata kwa hawa wanawake waliojifungua leo na wanaosubiri kujifungua. Hii yote ni katika kuutambua umuhimu wa mwanamke duniani,” alisema Jokate.
PICHA/STORI: GLADNESS MALYA/GPL