Lakini mchezaji huyo alipoonyesha hisani kama hiyo huko Misri katika runinga moja ya Misri wiki hii hatua hiyo lionekana na wengi kuwa matusi .
Wakati wa mahojiano ya runingani ''katika kipindi cha Yes am Famous'' kinachopeperushwa hewani na runinga ya MBC Misr,mchezaji huyo wa Argentina aliwaambia watangazaji hao kwamba angependa kutoa viatu vyake vifanyiwe mnada.
Kile ambacho Messi hakuelewa ni kwamba nchini Misri na mataifa mengine ya Uarabuni viatu hutumika kama ishara ya kukosa heshima ama hata matusi.
Hivyobasi raia wa taifa hilo walichukulia kitendo hicho kama makosa na kuanza kutoa hisia kali katika mitandao ya kijamii.
Image captionMbunge aliyetoa viatu vyake ili kumpatia Messi
Na ili kujibu matusi hayo mbunge mmoja wa Misri said Hassin anayetangaza kipindi kwa jina 'Infirad' alitoa kiatu chake na kusema kwamba atampatia Messi.
0 Comments