Meneja
Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha (Kulia) akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya udhamini wa Tigo wa kiasi cha Shilingi Milioni 11
katika kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO
WA KIJINSIA  ambayo inatarajiwa kuanza na
matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye
“Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 saa 12
asubuhi, katikati Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA),
Sadaka Gandi na kushoto  ni Rais wa  (TWA,) Irene Kiwia   ambao ndio waandaaji wa matembezi hayo,
kwenye mkutano uliofanyika mapema leo
jijini Dar es salaam.




Rais wa Taasisi
ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)
 Irene Kiwia  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu
udhamini wa Tigo katika  kampeni ya
kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake
Duniani,
inatarajiwa
kuanza na matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye  “Uwanja wa
Farasi ”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 kwenye 
mkutano uliofanyika mapema leo  jijini Dar
es salaam. 










Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF
ACHIEVEMENT (TWA),) Sadaka Gandi 
(katikati)  akifafanua jambo kuhusu  uzinduzi wa kampeni ya kampeni
ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA  kushoto kwake ni 
 Meneja Mawasiliano wa
Tigo John Wanyancha na kushoto kwake 
Rais wa 
Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) Irene Kiwia kwenye mkutano na waaandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar
es salaam.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Rais wa  TWA Irene Kiwia kuhusu udhamini wa Tigo katika  kampeni yakampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA  ambayo ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani katika mkutano uliofanyika mapema leo Jijini Dar es salaam .


Dar es Salaam, Machi
03, 2016
– Kampuni  ya Tigo Tanzania  imedhamini kampeni ya Kutaka Uwiano ambayo inatarajiwa  kuanza
na matembezi ya kilomita sita ambayo yataanzia kwenye “Uwanja wa Mbio za
Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi  5, 2016.
Kampeni hiyo imeandaliwa
na Taasisi ya Wanawake wenye Mafanikio (TWA) ambayo ni asasi isiyo ya kiserikali
ambayo lengo lake kuu ni kuimarisha ushiriki, na majukumu yawanawake na uwezo wao
katika jamii ya Tanzania kwenye mambo ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Kutoa    Ahadi ya Uwiano wa kijinsia ni kauli mbiu ya
mwaka huu katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Ambayo kilele chake
kitakuwa Machi 8, 2016.Kampeni ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa jinsia inatoa wito kwa
kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa uwiano wa kijinsia kwa
kasi zaidi ilikuwa saidia wanawake na wasichana kufikia  matamanio yao.
Matembezi hayo ya tafuatiwa
na Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Wanawake litakaofanyika kwenye Hoteli ya
Regency Kilimanjaro, Jumapili, Machi 6.
Akizungumza  kwenye mkutano  wa waandishi  wa habari leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano
wa Tigo, John Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali
Tigo inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wanawake ndani ya jamii na ndio maana  kampuni hiyo inaungana na watu wenye mapenzi mema
kuunga mkono kampeni  ya TWA.
 “Tigo inajivunia kuunga mkono TWA kwenye kampeni
hii ambayo ambayo inatafuta kuwawezesha wanawake kuingia kwenyeustawi wa wasaidie
wengine kustawi kwa ajili ya manufaa ya jamii. Ikiwa ni kampuni inayoendeshwa kwa
ubunifu, Tigo iko tayari kufanya kazi na watu wengine ambao ni  wabunifu, jamii, asasi zisizo za serikali,
serikali, sekta binafsi na za umma kwa ajili ya manufaa ya jamii yote,” alisema
Wanyancha.
Akitoa shukrani zake kutokana
na kuungwa mkono huko,Rais wa  TWA, Irene
Kiwia aliishukuru Tigo kutokana na kujikita kwake kusaidia mikakati mbalimbali ambayo
imejielekeza katika kuisaidia  jamii.

Kiwiaalisema, “Wakati tunakaribia
kuanza Kampeni ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa kijinsia,tunapenda kuishukuru Tigo
kwa ukarimu wake wa kutuunga mkono.

Bila uungwaji mkono wa kampuni
hii pamoja na huduma zake kubwa hatungeweza kufikia malengo yetu mengi katikakupanga
na kuandaa kampeni hii. Uungwaji mkono wa Tigo utakuwa na matokeo ya muda mrefu
yatakayowanufaisha wanawake kufuatia mafanikio ya kampeni hii.”

Hali kadhalika Kiwia alitoa
wito kwa watu kushiriki kwenye Matembezi ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa kjiinsia akisema,
“Tunatoa wito kwa watu binafsi, asasi zisizo za serikali, vyombo vya  habari, maofisa wa sekta  za umma na binafsi na wadau wengine kuja kwa wingi
na kuungana na sikushiriki kwenye matembezi na waalikwa kushiriki kwenye Mkutano
wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

NaibuWaziriWaAfya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Hamisi Kigwangala, atakuwa mgeni
rasmi katika matembezi   hayo.
Licha ya kutoa suluhisho
la kiteknolojia kidijitali la kisasa hapa nchini, Tigo kwa miaka mingi imekuwa ikisaidia
mikakati  ya kijamii ambayo yanaleta manufaa
makubwa kwa  jamii.

MWISHO