1
Kutoka kushoto ni Muigizaji mahiri wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’, Mkuu wa Masoko na mauzo wa Azam, Mrope Kiwanga, Msimamizi Uzalishaji wa kipindi cha Sinema Zetu Zamaradi Nzowa,  Mhadhiri Msaidizi wa UDSM Issa Mbura na Meneja mipango Fatma Mohamed, wakikata keki ya uzinduzi wa project ya Kiwanda cha Filamu naTamthilia ya Tax1 itakayorushwa  hewani kupitia channel 103 ya Sinema Zetu ya Azam TV ikiwa ni moja ya projekti mpya.

2
 Mkuu wa Masoko na Mauzo wa Azam, Mrope Kiwanga, akifafanua zaidi namna itakavyo nufaisha watu wengi project hiyo.
3
 Msimamizi Uzalishaji wa kipindi cha Sinema Zetu Zamaradi Nzowa akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa project hiyo.
4
 Muigizaji mahiri wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’, (kushoto) akimlisha keki msanii na mtangazaji mahari Bongo Daniel Kijo.
5
Baadhi ya waandishi wa habari na wahusika wa tukio hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
6
Muigizaji na Mhadhiri Msaidizi wa UDSM, Issa Mbura (kushoto) akimlisha keki Natasha.
7
Mwandishi wa gazeti la Championi Mohamed Mdose (kushoto) akilishwa keki na Natasha.
AZAM TV kupitia chaneli yake ya Sinema Zetu, mapema leo imezindua rasmi ‘projekti’ iliyopewa jina la Kiwanda cha Filamu, yenye lengo la kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo pamoja na wapiga picha za video chipukizi.
Projekti hiyo ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa Machi mwaka huu ilitoa furasa kwa watu mbalimbali ambao wangependa kushiriki kutuma kazi zao na waamepatikana zaidi ya washiriki 200.
Akizungumza nawanahabari katika uzinduzi huo kwenye Ofisi za Azam Tazara jijini Dar, Msimamizi wa Uzalishaji wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa, alisema washiriki hao watawachuja chini ya majaji akiwemo muigizaji wa siku nyingi hapa nchini, Suzan Lewis ‘Natasha’ ili kuwapata 22.
Baada ya kupatikana watapatiwa mafunzo mafupi kisha wao pamoja na mastaa wa filamu hapa nchini watashiriki kwenye tamthilia itakayojulikana kwa jina la Taxi.
Nzowa alisema: “Washiriki ni kuanzia umri wa miaka 18 na kesho Jumatano pale Coco Beach ndipo tutaanza kufanya mchujo wa awali ambapo mpaka mwisho tunatarajia kupata waigizaji 20 na wapiga picha wawili ambao watashiriki kwenye tamthilia ya Taxi ambayo itazinduliwa Julai mwaka huu na itakuwa ikionyeshwa katika chaneli yetu ya Sinema Zetu,”
Picha: Musa Mateja/GPL.