DAU-600x360
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dkt. Ramadhani Dau.
NA MWANDISHI WETU Risasi Jumamosi
“Hili jambo halikubaliki na kama tuhuma hizi ni za kweli, basi tunamuomba Rais John Magufuli amchukulie hatua za kisheria kama wanavyofanyiwa wakubwa wengine waliolitia taifa letu hasara. Hiki ni kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingeweza kutumiwa kutatua kero mbalimbali zinazotukabili Watanzania,” alisema msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Seve Nyari kutoka Singida.

Joji Salum, aliyepiga simu kutoka Kigamboni, Dar alisema ni kweli mradi wa ujenzi wa Jiji Jipya la Kigamboni umesimama na hawajui ni kwa sababu gani, lakini kwa ufisadi wa fedha zinazotajwa, hakuna jinsi zaidi ya kumsulubu Dau ambaye aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa balozi lakini bado hajapangiwa kituo cha kazi kwa sababu alishiriki kwa asilimia mia moja si kwa kuzichukua bali kama mtendaji mkuu.
Kutoka Arusha, ambako NSSF inaendelea na mradi mwingine wa ujenzi wa nyumba wilayani Arumeru, Maige Joseph alisema:
Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi SaidRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
“Wakati umefika kwa mifuko ya jamii kama huu, kudhibitiwa katika uanzishaji wa miradi yake, kwani mingi ni ya kifisadi yenye kuwanufaisha wakubwa.
“Sasa mtu una ardhi yako, lakini unanunua tena ya mtu mwingine, tena kwa bei ghali zaidi. Yaani unatoka kilometa 30 kutoka Arusha mjini, unakwenda kununua heka moja kwa shilingi bilioni moja!? Hii haijapata kutokea, labda Tanzania tu. Wasulubiwe walioshiriki,” alisema Maige.
Akaongeza: “Nasema Dau anahusika kwa sababu si ndiyo alikuwa bosi mkuu? Maana yake ni kwamba hakuna kilichokuwa kikifanyika bila ya yeye kujua. Ni lazima anajua mwanzo mwisho. Mimi naona hata huo ubalozi ungetenguliwa tu kwani ameacha doa NSSF.”
Kauli ya kutaka watu wote waliohusika kufisadi fedha hizo wasubulubiwe, pia ilitoka kwa wananchi waliopiga simu kutoka Mwanjelwa Mbeya, Tukuyu (pia Mbeya), Iringa mjini, Mtwara, Simiyu, Kondoa (Dodoma), Tanga na Mwanza.
Ufisadi ulioibuliwa hivi karibuni ni kiasi cha shilingi trilioni 1.3 kinadaiwa kutumiwa na NSSF katika mazingira yanayotia shaka katika ununuzi wa ardhi ili kutekeleza miradi miwili ya ujenzi wa nyumba huko Kigamboni na Arumeru mkoani Arusha. Jijini Dar es Salaam, mfuko huo ulianzisha mradi uitwao Dege Eco Village ambao Bodi ya NSSF iliunda Kampuni ya Hifadhi Builders inayosimamia ujenzi huo ikishirikiana na Kampuni ya Azimio Housing Estate Limited.
Mafuta_House_(cropped)
Inadaiwa Azimio Housing Estate inayomiliki ekari 20,000 huko Kigamboni, iliiuzia NSSF eneo la ekari 300 kwa shilingi milioni 800 kwa ekari moja, badala ya bei halali ya shilingi milioni 39 kwa ekari tofauti na bei iliyotangazwa na Manispaa ya Temeke mwaka 2012 wakati ikiuza eneo lake kwa shilingi elfu nane kwa mita ya mraba.
Katika ujenzi wa Arumeru, inadaiwa kampuni hiyo ya Azimio, iliiuzia NSSF ekari moja kwa shilingi bilioni 1.8, wakati bei halisi ya ukubwa huo kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo lililo umbali wa zaidi ya kilometa 30 kutoka jijini Arusha, ni kati ya shilingi laki tano hadi milioni moja.
Uchunguzi unaonesha Azimio iliuza eka 300 za Kigamboni kwa dola 108, 906,113 (sawa na madafu bilioni 217.8), wakati huko Arumeru mfuko huo uliuziwa ekari 655 kwa dola 556, 764, 924 (trilioni 1.13) na hivyo kuifanya jumla ya fedha ambazo ‘zimeliwa’ katika miradi hiyo miwili katika ardhi peke yake kufikia trilioni 1.3.