john-magufuliRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’.
STORI: Sifael Paul, Wikienda
Dar es Salaam: Hali ni mbaya! Vita ya ufisadi aliyoitangaza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ inadaiwa kuwalaza njaa wapiga dili mjini na madalali waliokuwa wamejazana kwenye taasisi za serikali.

Uchunguzi wa gazeti hili kwenye taasisi kubwa zipatazo 20 zilizopo katika wizara mbalimbali zenye makao yake makuu jijini Dar, umebaini kuwa, wale ‘watu wa kati’ kwa sasa hawana dili kwani JPM ameziba mianya yote ya rushwa.
“Kama alivyosema Ludovick Utouh (aliyekuwa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali) kuwa serikali na taasisi zake ilikuwa imejaa madalali na mafisadi ni ukweli mtupu.
“Ilikuwa ni vigumu kupatiwa huduma bila kujuana au kuwepo kwa mtu wa kati aliyekuwa pale kwa ajili ya kukamilisha dili, lakini sasa wanapiga tu miayo mitaani. Kweli JPM amenyoosha watu,” alisema mmoja wa wananchi waliojitokeza kupata huduma kwenye Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na kudakiwa na mwingine:
“Kwenye mashirika ya umma hali ilikuwa mbaya mno.
Ndiyo maana tunasema JPM aachwe akomeshe watu kwa sababu ameachiwa nchi iliyooza, yenye sera mbovu za kukumbatia na kuruhusu wapiga dili kuliibia taifa.”
Miezi kadhaa baada ya kuishika nchi, Rais Magufuli alikuwa na kazi kubwa ya kupanga mikakati ya kuijenga Tanzania mpya kwa kupiga vita ufisadi hivyo hata kama kuna wachache wanaolala njaa kwa mkakati wake huo ni heri walale njaa lakini Watanzania walio wengi wapate neema.