Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 22, 2016

Mwanamuziki maarufu Prince amefariki

Mwanamuziki kutoka Marekani maarufu kwa muziki wa chapa Funk, Prince ameaga dunia.
Mwanamuziki huyo raia wa Marekani alipatikana ameaga dunia katika makazi yake ya huko Minneapolis.

Image copyrightGetty
Image captionPrince
Alikuwa na umri wa miaka 57.
Prince alitawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 70 na themanini kwa vibao vyake maarufu kama vile 'I Wanna Be Your Lover' na 'Little Red Corvette'.
Anasifika kwa ubunifu wake wa kutajika na kwa midundo iliyowaongoa wapenzi wa muziki kote duniani .
Image copyrightGetty
Image captionPrince alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na , funk na psychedelia''.
Prince alibuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na , funk na psychedelia''.
Muziki wake ulikuwa maarufu kiasi ya kwanza aliwahi kuuza takriban albamu milioni 100.
Kipawa chake kilimwezesha kutunga kusanifu kutayarisha na pia kuimba nyimbo zake mwenyewe.
Image copyrightGetty
Image captionPrince alitawala chati za muziki kote duniani katika miaka ya 70 na themanini
Vile vile aliwatungia nyimbo waimbaji wengi tu kote duniani.
Yamkini msanii huyo nguli alikuwa anaugua kwa kipindi kirefu na hata alilazimika kukatiza Shoo zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP