OTH_5539
Meneja Mradi kutoka NSSF, Mhandisi Karim Mataka amesema baadhi ya Madereva wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na alama zilizowekwa katika daraja la Kigamboni ambalo ni kubwa Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 100 iwapo litapata matunzo stahiki.

Mhandisi Karimu amebainisha kuwa magari yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe chini ya tani 10, kwa sababu kwa upande wa Kigamboni bado baadhi ya barabara hazijakamili, hivyo ni vyema Madereva wote wakawa makini.
Daraja hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016, Mhandisi Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji matunzo.
Mhandisi alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)