Rais wa Marekani Barack Obama amasisitiza kuwa Uingereza itapoteza ukuaji na ushawisi wake iwapo itaamua kuondoka katika muungano wa Ulaya kupitia kwa kura ya maoni mwezi Juni.

Akiongea baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron mjini London, Obama alisema kuwa Uingereza itakuwa nyuma katika kuafikiana mikataba ya kibiashara na Marekani ikiwa itaondoka.
Wale wanaounga mkono kuondoka kwa Uingereza wamekosoa hatua za rais Obama za kuingilia kati suala hilo.
Obama hatahivyo amesema kuwa hakuwa na nia ya kushawishi kura bali kuongea ukweli kama rafiki.