Kiongozi wa mashtaka nchini Argentina ameomba idhini ya mahakama kuanzisha uchunguzi katika shughuli za aliyekuwa rais wa taifa hilo, Cristina Fernandes de Kirchner, juu ya madai kuwa alishiriki katika utakasaji wa pesa haramu.
Uamuzi huo unafuatia ushahidi uliotolewa mahakama Ijumaa na mfanya biashara, Leonardo Farina mshirika wake yeye na mumewe ambaye pia alikuwa ni rais wa Argentina bwanaNestor Kirchner .
Akitoa ushahidi baada ya kuahidiwa kusamehewa makosa yake mfanyabiashara huyo alisema kuwa Bi Fernandez na marehemu mumewe Nestor Kirchner walishiriki katika shughuli kadhaa ya ulaghai wa fedha za umma.
Image copyrightGettyImage captionUchunguzi huo unatokana na ufichuzi uliotokea kwenye kampuni ya Mossack Fonseca
Mfanyabiashara mwingine ambaye pia ni mwandani wa familia ya Kirchner, Lazare Baez, alitiwa mbaroni mapema juma lililopita na kulaumiwa kwa ulaghai wa Dola Milioni tano
0 Comments