Takriban watu 260,000 wamelitoroka taifa la Burundi tangu kuzuka kwa mgogoro mwaka mmoja uliopita,huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka hadi 330,000 kufikia mwisho wa mwaka ,iwapo suluhu ya kisiasa haitapatikana na ishara za kuzuka kwa vita vya wenyewenye kwa wenyewe kutositishwa.

Kulingana na tume ya wakimbizi katika shirika la umoja wa Mataifa UNHCR wengi wa wakimbizi waliotorokea katika mataifa jirani wamelalamikia unyanyasaji ,wa kingono kukamatwa mara kwa mara,vitisho,kuajiriwa kujiunga na jeshi na mauaji.
Tanzania ina idadi kubwa ya wakimbizi wakiwemo raia 30 wa Burundi wanaoingia nchini humo kila siku na kambi ya Nyarugusu ni miongoni mwa kambi kubwa duniani ikiwa na wakimbizi 140,540.
Tume hiyo imesema kuwa idadi nyengine ya wakimbizi katika mataifa mengine ni kama ifuatavyo:
Rwanda (76,404)
DRC (22,204)
Uganda (24,583).