Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 21, 2016

Vurugu zaendelea nchini Zambia

Polisi nchini Zambia wamesema watu wawili wamechomwa moto mjini Lusaka katika vurugu ya ubaguzi wa wenyeji dhidi ya wageni.
Watu Zaidi ya mia mbili na hamsini wamekamatwa baada ya maduka mengi yanayomilikiwa na wanyaruanda kuvamiwa.Uvamizi huo ulitokea baada ya wanyaruanda kushutumiwa kuua watu na kutumia viungo vyao kuvutia wateja.

o Padre Charles Chilinda ameiambia BBC kuwa kanisa lake linafanya jitihada zote ili kuweza kuwasaidia wahanga ambao wamekwenda kuomba hifadhi kanisani.
"Kitu ambacho tunaweza kuwapa ni kwamba watakuwa na usalama wa kutosha kuwa hapo,tutaenda kuwaangalia na kuwaeleza kuwa hawa sio wazambia ambao wanagombana nao.hali hii haikubaliki ,kila mtu aliyepo katika ardhi ya Zambia analindwa na katiba ya Zambia.Ni jukumu letu kudumisha Amani na tushirikiane katika kulitokomeza hili"

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP