Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Apr 27, 2016

Wanamuziki, wadau kukutana na Makonda

Paul-Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda.
WANAMUZIKI wa dansi, taarab, Bongo Fleva na wadau wa muziki waishio Dar es Salaam, Alhamisi hii watakutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda, ili kubadilishana mawazo juu mwenendo wa kazi zao.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kuanzia saa tano ili kujadili changamoto za Sheria ya Biashara ya Vileo na Burudani ambayo iko tangu mwaka 1968 na 1972.
MakondaMmoja wa wasemaji wa umoja huo, Juma Mbizo, ameuambia mtandao huu kuwa maombi yao ya kumwalika Makonda yameshawasilishwa kwake.
Mbizo amesema mkutano huo hauhusiani na chama chochote cha muziki, bali umeandaliwa na waathirika wakuu wa sheria hiyo.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP