Wananchi wa Kigogo wanufaika na upimaji bure wa afya kutoka Fazel Foundation na TAHMEF
Na Rabi Hume, MoDewjiBlog
Kwa kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Zoezi hilo lilifanyika Aprili, 23 katika Msikiti wa Al Ghadir uliopo Kigogo Post na jumla ya 352 wanawake wakiwa 150 na wanaumme 202 walipimwa Malaria, Kisukari, Shinikizo la Damu na Upungufu wa Damu mwilini.
Kati ya watu hao, watu 38 wameonekana kuwa na Shinikizo la Damu, 36 Upungufu wa Damu, 8 Kisukari na mmoja Maralia ambapo walipata nafasi ya kupatiwa dawa na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali.
Aidha kwa mafanikio hayo, Fazel Foundation inawashukuru wote walioshiriki katika huduma hiyo akiwepo Dkt. Mohammed Alloo, Dkt. Sibtain Moledina, Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL Group), Salama Pharmaceuticals na Clinicheck Labs, Imam wa msikiti wa Al Ghadir Sheikh Jalala, Msikiti wa Al Ghadir, Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Team ya Volunteers na Hawza ya Imam Sadiq kwa ushiriki wao katika zoezi hilo.
Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel akisalimiana na Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama wakati wa funguzi wa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Katikati ni Imam wa Msikiti wa Al Ghadir , Sheikh Jalala. (Picha zote na Rabi Hume - modewjiblog.com)
Wakiwa katika picha ya pamoja, Wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama, Imam wa Msikiti wa Al Ghadir , Sheikh Jalala, Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel na Mwanzilishi wa Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF), Juliana Busasi.
Boniventure Pius akimpima Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala wakati wa uzinduzi wa upimaji afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Aliyesimama kulia ni Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel.
Mkisi Shamra akimuhudumia mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Mary Kalleku akimpima mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Victoria Msambichaka akimwambia jambo mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliofika kupimwa afya bure kutoka Fazel Foundation na TAHMEF.
Eneo lililokuwa likitumika kupokea wananchi waliokwenda kupima bure afya zao.
Dkt. Mohammed Alloo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akimshauri jambo mmoja wa wananchi waliofika katika kituo kilichokuwa kikitumika kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo, Dar es Salaam.
Alex Juma akimpa dawa mmoja wa wananchi aliyefika kupima afya bure baada ya kubainika kuwa na ugonjwa.
Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel akizungumza jambo na Mwanzilishi wa Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF), Juliana Busasi wakati wakati zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Kigogo likiendelea.
Kenneth Mananu akimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika kituoni kupata vipimo vya afya bure. Anayefuatia ni Joshua Mnkeni akimpa ushauri mmoja wa wananchi aliyefika kupata huduma ya kupima afya bure.
Eneo la kutolea huduma kwa wananchi wanaofika kupata huduma.
Wagonjwa wakisubiri kumuona daktari.
Hans Olomi akimpima mmoja wa watoto waliofika kupimwa afya zao bure, Anayefuatia ni Simon Nassary.
Mwanzilishi wa Fazel Foundation, Dkt. Sajjad Fazel akimwambia jambo Kenneth Munanu wakati zozi la upimaji likiendeea.
0 Comments