Mashirika ya msaada nchini Yemen, yameonya matokeo yanaweza kuwa mabaya sana, iwapo makubaliano ya kusitisha mapigano, yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, hayatotekelezwa leo kuanzia leo.
Taarifa ya mashirika ya misaada 16 pamoja na Oxfam, Islamic Relief na Save the Children inasema kuwa watoto 137 wanakufa kila siku, kutokana na magonjwa yanayoweza kutibiwa.

Image copyrightEPA
Image captionWaasi wa- Houthi
Mashirika hayo yanasema, karibu watu milioni 3 wamehama makwao tangu vita vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya wapiganaji waasi wa- Houthi, kuanza mwaka mmoja uliopita.