Kama kawaida, Kampeni ya "Raha yako ya Rock City ni nini"? inayoendeshwa na 102.5 Lake Fm, Raha ya Rock City #RadioYaWananzengo iliyopo Jijini Mwanza, inaendelea.
Katika kampeni hiyo, wasikiliza hufuatwa huko huko waliko na kueleza raha zao na kisha kutwanga fotoo ambazo huwekwa mitandaoni ili kushare na wengine. Wiki hii, Wasomi Kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino #Saut Mwanza wametisha sana.
Ukitembelea mitandao ya kijamii Instagram, Facebook na Twitter @lakefmmwanza utaona ambavyo #Saut wametisha ambapo mfano mzuri ni hiyo picha hapo juu. Kumbuka 102.5 Lake Fm bado iko katika matangazo ya majaribio ila ujio wake ni wa kasi ya ajabu.
0 Comments