Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 2, 2016

KESSY: WABUNGE WAPENDA RUNINGA NENDENI SALUNI

 
kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu
Shaka akiwa ananyesha baadhi ya kadi za chadema ambazo zilirudishwa
katika mkutano huo wa adhara

 Kaimu
Katibu Mkuu Uvccm Taifa Ndg SHAKA HAMDU SHAKA awataka viongozi wa
jumuiya kujifunza KUTOKA wilaya za SAME na SIMANJIRO kwa ufanisi na
ubunifu wa kuongoza Jumuiya

Na Woinde
Shizza,Kilimanjaro


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Same Mkoa Kilimanjaro Augostino Kessy
amewataka wananchi wapenda amani na maendeleo ya kweli kuwapuuza wabunge
wa upinzani waliokwenda bungeni badala ya kuwawakikisha wananchi
wameamua ili waonekane kwenye runinga .


Amesema aina ya wabunge hao wameshindwa aidha kujua majukumu yao ya
kuwepo kwao bungeni au wanataka waonekane kwenye TV bila kujali gharama
zinazopunguza kujehgeka kwa ustawi wa uchumi wa wananchi hasa wanaoishi
vijijini.


Kessy alitoa matamshi hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya stendi ya mabasi Same Mjini mkoani humo.


Alisema ni aibu na fedheha mpya kusikia wabunge ambao wamepewa dhamana
ya kuwatumikia wananchi wakikataa kushiriki vikao vya bunge hadi
waonekane kwenye runinga.


"Huu ni upuuzi wa kisiass na utoto wa mwisho wanaoufanya wabunge wa
upinzani, kama hawajui dhamana walionayo wakajifunze ccm, kama wanataka
ubishoo basi  waende saluni "alisema


Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM  wilaya Same alisema vyama vya upinzani
licha ya kukosa sera, dira na mipango vyama hivyo baadhi ya viongozi na
wabunge wake hawana busara na si wazalendo.


Mapema Kaimu Katibu wa UVCCM wilaya same Neema Msangi alisema anaamini
vijana wote waliosukunwa na upepo  yabis na kuhamia vyama vya upinzani
bado wana nafasi ya kurejea na kupokelewa kwa heshima.

 Neema alisema
viongozi wa upinzani ikiwemo ule umoja bwa ukawa hawakuwa na  mipango
wala uwezo kuongoza Taifa ila walichokuwa wakikitafuta ni tsmaa ya
madaraka,umaarufu na uroho wa fedha.


Hata hivyo katika hali ambayo haikutazamiwa na wananchi wengi wakaazi wa
mji mdogo wa same ni mwanachama mfurukutwa wa chadema Amani Joseph
Mgonja kukihama chama hicho na kujiunga na ccm.


Akizungumza katika mkutano huo mara baada ya kuchukua kadi ya ccm Mgonja
alisema hakutaka chadema kwa bahati mbaya ila amekipima na kukichambua
chama hicho na kukuta hakina malengo ya kujijenga kama taasisi ya
kisiasa.


Kaimu katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka aliwabeza wanasiasa wa
upinzani ambao wanapita huku wakisema anachofanya Dk John Magufuli ni
kutekeleza ilani ya ukawa.


Alisems Dk Magufuli hakunadi ilani yenye sera za majimbo zenye lengo la
kuigawa nchi kwa ukanda ,ukabila na uzawa ambayo alisema wananchi ikiwa
wataingia kwenye mtego huo  wataitumbukiza shimoni na kuiletea
majanga.


"Tumeishi kwa miaka 52 wote ni ndugu wa tumbo moja hakuna anayembagua
mwenzake kwa rangi au kwa kabila lake, wanachotaka kukipandikiza chadema
ni kulipasua Taifa".


Jumla ya wanachama 132 wa uvccm,ccm ,  chipukizi wa ccm na UWT walipewa
kadi mpya na shaka ambaye yuko wilayani same kwa ziara ya kutazama
utekekezaji wa ilani ya uchaguzi na uhai wa uvccm.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP