Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 2, 2016

MAZIKO YA MTOTO COMFORT.. NI SIKU YA JUMATANO TAREHE 04.05.2016 NCHINI UBELGIJI

Ndugu Jesse wa Boom   anapenda kuwatangazia Waafrika wenzake wote wa Ubelgiji na nchi zilizo jirani kuwa mazishi ya mpwa wake Comfort yatafanyika siku ya jumatano ya tarehe 04.05.2016 saa saba kamili.
Mtoto Comfort ataagwa Mochwari saa sita kamili mchana  na anuani  ya kufika hapo Mochwari ni kama ifuatavyo: Oosterveldlaan 24,Post code 2610 Wilrijk,Sint-Augustinus.
Baada ya kuagwa watu wataelekea makaburini kwa ajili ya kumstiri mtoto Comfort,Anuani ya Makaburini ni kama ifuatavyo:
Kerkhofstraat 386
2850 Boom.


Kwa watakaotumia usafiri wa Bus Wapande Bus wakitokea Boom Market bus no 182
linalokwenda Groenplaats na kituo cha kushuka kinaitwa Kerkhofstraat.

Shime ndugu wapendwa wote,tunawaomba tujumuike katika kumstiri mtoto Comfort katika nyumba yake ya milele.Tunaomba sana kila atakayeliona tangazo hili amfahamishe na mwenzake.
Shukrani.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP