Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve akifurahi jambo na wakinamama wenye ulemavu.




 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve akizungumza na wanawake wa chama cha mapinduzi ccm mkoani iringa.

na fredy mgunda,iringa

Wananchi mkoani iringa wanatarajia kunufaika na muungano
wa wabunge watatu vijana wa viti maalu kwa lengo kubadilishana uzoefu wa
kuwaletea maendeleo wanawake wa mkoa huu.

Akizungumza na blog hii Mbunge wa viti maalum mkoa wa Rose Twelve alisema wameamua
kuungana ili kubadilisha mfumo wa utawala na kuondoa ufanyaji wa kazi kwa
mazoea sambamba na kuwasaidia wananchi wanaowatumikia.

“Unajua kuwa changamoto na matatizo ya wanawake kwa
asilimia kubwa zinafanana hivyo najifunza kwa wenzangu wanatatuaje changamoto
hizo ili na mimi niweze kutatua matatizo ya wanawake wa mkoani iringa na
waendelee kufanya maendeleo huku wakiwa hawana changamoto nyingi”alisema Rose

Aidha rose aliongeza kwa kusema kuwa kiongozi bora ni
Yule aliyetari kujifunza ili aweze kupata ujuzi wa kuwasaidia wananchi kwa kuwapa
mbinu wananchi za kuwaletea maendeleo.

Rose alisema amejipanga kuwekeza kwenye elimu ili kuwapa
wanawake fursa ya kuwapa ya kuwawezesha kunufaika na mfuko wa mbunge
anaotarajia kuuanzisha.

“Nitatoa milioni hamsini kila mwaka kwa umoja wa wanawake
wa ccm UWT mkoani hivyo lazima nitafute njia mbadala ya kuwapa elimu ya
kuzitumia hizo pesa ili ziwanufaishe kwa kuwaletea maendeleo”.alisema Rose

Lakini Rose alisema kuwa atataufa wataalamu wa mafunzo
mbalimbali ili wanawake wa mkoa wa iringa wapate elimu ya ujasiliamali na
kuokoa pesa ambazo zimekuwa zikipotea.

Nitatafuta wadau mbalimbali wachangie mfuko wangu wa
mbunge kwa lengo la kuwasaidia wanawake ambao hawana mitaji ya kujiendesha
maisha yao.alisema Rose

Amemalizia kwa kuwataka wakazi wa Iringa kufanya kazi kwa
bidii ili kuleta maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.