Kulia ni Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) na Kushoto ni meneja wa msanii huyo, Hemed Kavu. Snura amesema kuwa yupo tayari kufanya upya video ya Wimbo wake wa chura ambayo itafuata maadili ya kitanzania kwani tayari ameshachukua vibali vya kufanya upya video ya wimbo huo.
Msanii Wa Bongo Movie Snura Mushi (Snura) amewaomba radhi watanzania kwaujumla pamoja na vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutokufuata sheria na kanuni na taratibu zilizopo katika uendeshaji wa sanaa.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, radhi hiyo imekuja mara baada ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo jana kufungia video ya wimbo wa msanii huyo wa Chura ikiwa ni pamoja na kutoonyeshwa kwenye Televisheni pamoja na kupigwa kwenye redio. Amesema kuwa tayari video ya wimbo huo ameshatoa kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube. |
0 Comments