Sehemu ya Wakimbiaji wa Mbio za Mwenge, wakiwa tayari kuupokea Mwenge huo ulipowasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016. Zaidi ya vijana 40 waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya Madawa ya kulevwa wanalelewa katika kituo hicho.Picha zote na Othman Michuzi - MMG.
 Mmoja wa wakimbiza Mwenge huo, akiongoza mbio hizo wakati Mwenge wa Uhuru ulipokuwa ukiwasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016.
 Mwenge umehifadhiwa kwenye sehemu yake.
Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (hayupo pichani) wakati Mwenge huo ulipotembelea kituo hicho Mei 19, 2016.
Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji (kulia)  akikikabidhi taarifa hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima, mara baada ya kuisoma.
Mmoja wa Vijana waliokuwa wameathiriwa na Madawa ya Kulevya ambaye sasa amerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kupatiwa tiba aliefahamika kwa jina la Abdullatif, akisoma ngonjera aliyoiandaa mwenyewe yenye ujumbe wa kuwataka vijana wengine kuachana kabisa na matumizi ya madawa ya kulevya, kwani yanaathari kubwa kwao.
Abdullatif akimtabithi Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima ngonjera yake hiyo.

Sehemu vijana waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya wakifatilia hotuba mbali mbali zilizokuwa zikitolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga akizungumza machache wakati wa halfa hiyo ya Mwenge kutembelea katika Kituo cha Bagamoyo Sober House.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima akitoa hotuba yake ambapo aliwataka vijana hao walioamua kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na kurudi katika shughuli za ujenzi wa taifa, kwani vijana ni nguvu kazi ya taifa.
Picha ya pamoja na baadhi ya vijana hao.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (kushoto) akimkabidhi Mwenge, Mmiliki wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, wakati wa hafla fupi ya Mwenge huo ulipotembelea kituo chake hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga.