Rais wa kwanza wa kike wa Taiwan, ameapishwa Ijumaa katika sherehe zitakazofanyika katika mji mkuu wa Taipei. Tsai In-wen, ambaye chama chake kinataka uhuru kutoka Uchina, alishinda na idadi kubwa ya kura katika uchaguzi uliofanyika Februari mwaka huu. Ushindi wake umepunguza uhusiano wa taifa hilo na utawala wa Beijing.

China inadai kuwa Taiwan ni Mamlaka yake na kutokana na hatua ya sasa ya Taiwan na hata wakati wa Uchaguzi,China imeonekana kutokubalianana Taiwan.
Tsai anakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kushuka kwa mapato yatokanayo na usafirishaji wa bidhaa nje.