Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 29, 2016

REAL MADRID MABINGWA WAPYA 2016-2017 UEFA,YAIFUNGA ATLETICO MADRID KWA PENATI

Sergio Ramos akishangilia bao lake la kwanza dakika ya 15 ya mchezo dhidi ya Atletico Madrid katika fainali za klabu bingwa barani ulaya.Real Madrid wameibuka kidedea kwa kuunyakuwa ubingwa huo wa UEFA baada ya kuifunga Atletico Madrid goli 5-3 kwa njia ya penati baada ya kumaliza dakika 120 kwa sare ya 1-1

Mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos kulia akiandika bao la kwanza dakika ya 15 ya mchezo dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa fainali za UEFA uliochezwa Milano nchini Italia.

Yannick Carrisco wa Atletico Madrid akiweka bao kimiyani na kuisawaizishia timu yake dhidi ya Real Madrid na kuwa 1-1 

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Yannick Carrasco akishangilia bao la kusawazisha dhidi ya Real Madrid katika fainali za UEFA zilzofanyika Milano nchini Italia.Goli lake alilifunga dakika ya 79 kipindi cha pili na kufanya timu kwenda sare ya goli 1-1 mpaka mwisho wa mchezo kabla ya kupigwa penati baada ya dakika za nyongeza kwisha.

Mshambuliaji wa timu ya Real Madrid Christian Ronaldo akivua jezi kwa furaha baada ya kuifungia timu yake goli la ubingwa dhidi ya timu ya Atletico Madrid.

Shingo chini ikiwa ni ishara ya masikitiko makubwa kwa mchezaji wa Atletico Madrid, Juanfran baada ya kukosa penati ya nne kwa timu yake.

Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia ubingwa wao kwa kila mmoja kumkimbilia Christiano Ronaldo baada ya kuifungia bao la mwisho la penati ya mwisho na kuifanya Real Madrid kuwa mabingwa kwa jumla ya goli 5-3.Timu zote zilitoka sare ya goli 1-1 ndani ya dakika 90 za kawida na baadae kuongezewa dakika za nyongeza 30.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP