Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 23, 2016

TANZIA: Ras BUPE BAKWERESA KARUDI AFARIKI DUNIA


Habari za uhakika na kusikitisha zimetufikia kuwa mwanaharakati Ras Bupe Bakweresa Karudi maarufu pia  kama kaka Bupe Mkushi,amefariki dunia katika hosptali ya taifa muhimbili baada ya kupata ajari ya gari.
Ras Bupe ameacha mke na watoto, mke na mtoto wake wa kiume ameshawasili nchini kutokea Uingereza.msiba hupo karakata jijini Dar-es-salaam.Marehemu Ras Bupe Bakweresa Karudi alikuja nchini Tanzania katikati mwa miaka ya 70 akifuatana na mkewe na watoto wawili Kiyenda(msichana) na Nyamiche mvulana,Ras Bupe Karudi alikuja kumuomba marehemu baba wa taifa mwalimu Nyerere hili atoe idhini
kwa watu weusi wa visiwa vya Karibiki warudi Afrika(Tanzania) kama 
nyumbani kwani ndio asili yao,baada ya kukubaliwa maombi yake,
Marehemu Bupe akaungana na wanaharakati wenziwe hapa nchini
wakiwemo marehem Prof.Joshua Mkhululi aka Prof.Keneth Eduward
na Marehem Ras Kwetenge Zanaki Sokoni (wajamaika),wengine ambao
wapo hai Mani Imani wakaungana na wenyeji wao Said Jazbo Vuai,Isza Suleiman na Ebrahim Makunja au Kamanda ras Makunja wakasajili
chama cha ushirika chenye jina la UHURU,UMOJA NA MAENDELEO
chenye makao kule mbezi beach,wakiwa wanajishughulisha na mipango ya kilimo na kumiliki maroli ya usafirishaji. Marehem Kaka Ras Bupe atakumbukwa sana kwa harakati zake zake za kuupigania uafrika na kuwahamasisha raia wenye asili ya kiafrika kurudi Tanzania.
Mungu mlaze pema peponi marehemu Bupe Bwakweresa Karudi 
Amen
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP