Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

May 7, 2016

TAZAMA VIDEO YA MCHEZAJI WA CAMEROON ALIVYOANGUKA UWANJANI NA KUPOTEZA MAISHA

Mchezaji wa klabu ya Dinammo Bucharest ya Romania raia wa Cameroon, Patrick Ekeng, 26 ameanguka uwanjani na kupoteza maisha wakati timu yake ikicheza mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Viitorul Constanta.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya goli 3-3, Ekeng alianguka dk. 69 ambapo mchezo ulisimama kwa dakika saba ili kupisha wahudumu wa afya kuona ni jinsi gani wataweza kuokoa maisha yake lakini ilishindikana.
Hali ya huzuni ilitawala zaidi baada ya Msemaji wa Hospitali ya Floreasca, Cristian Pandrea kutoa taarifa za kifo cha Ekeng na kueleza kuwa madaktari walijitahidi kuokoa maisha ya Ekeng bila mafanikio.
gettyimages-528662762Patrick Ekeng akiwa chini baada ya kuanguka wakati mchezo ukiendelea.
Mchezaji huyo wa Cameroon alikuwa akiishi Romania na mke wake pamoja na motto wake wakiishi Paris, Ufaransa na kuna taarifa kuwa alikuwa aende Ufaransa kuungana na familia yake siku ya Jumanne baada ya fainali ya Ngao ya Hisani nchini humo. Mke wake anatarji kuwasili Romania leo Jumamosi.
Ekeng anakuwa siyo mchezaji wa kwanza wa Dinammo Bucharest kwani hata Octoba, 2000 aliyekuwa nahodha wa timu hiyo, Catalin Hildan alianguka na kupoteza maisha.


Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP