Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 18, 2016

Auawa akiwa katika facebook Live-stream

Mtu mmoja nchini Chicago alipigwa risasi akiwa katika video ya moja kwa moja inayojulikana kama Live_stream katika mtandao wa Facebook ,polisi wamesema.
Antonio Perkins mwenye umri wa miaka 28 alipigwa risasi katika kichwa na shingo magharibi mwa mji huo.

Kanda hiyo ya video bado iko katika facebook na imeangaliwa mara 700,000.
Ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu mjini Chicago ambapo mauaji yamefanyika moja kwa moja katika mtandao wa facebook.
Mnamo mwezi Machi mtu asiyejulikana alipigwa risasi mara 16 wakati akipeperusha matangazo hewani.
Hakuna mtu aliyekamatwa kufika sasa.Programu ya live-streaming ya facebook inawaruhusu watu kutangaza moja kwa moja mtandaoni

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP