Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.
Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.

Image captionWafuasi wa Bemba wakifutilia hukumu kutoka DRC

Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.
Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.

Jean Pierre Bemba

Makamu wa rais wa zamani DR Congo

18
Miaka ambayo amefungwa jela na ICC
  • 2002-2003 Kipindi ambacho anadaiwa kutekeleza uhalifu CAR
  • 2008 Mwaka aliokamatwa Brussels