Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 21, 2016

Bungeni Dodoma: Ukawa kama kawa!

Dodoma-UKAWA kama kawa: Ndiyo lugha nyepesi tunayoweza kusema, hii ni kutokana na Wabunge wa Kambi ya Upinzani kuendelea kususia vikao vya bunge baada ya leo kutoka tena nje ya ukumbi huo kimya kimya wakisusia kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dkt.  Tulia Ackson.

Wabunge hao leo wametoka bungeni bila mbwembwe kama za jana ambapo waliziba midomo yao kwa karatasi na utepe kisha kutoka nje ya ukumbi wa bunge hilo mjini Dodoma.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema kuwa, kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo (UKAWA) imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao bungeni na kwamba watatoa taarifa kamili baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP