Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 9, 2016

Kambi ya wanajeshi wa AU yashambuliwa Somalia

Wanajeshi tisa wa Muungano wa Afrika wameuawa na wengine sita kujeruhiwa wakati wa shambulizi lililoendeshwa na wanamgambo wa kiislamu wa al-Shabab katika moja ya kambi zake.

Waziri wa ulinzi nchini Somalia Abdirisak Omar Mohamed, alikiambia kituo cha radio cha serikaili kuwa, wanamgambo 240 waliuawa wakati wa shambulizi hilo.
Kwa upande wake al-Shabab wanasema kuwa wamewaua wanajeshi 60 wakati wa shambulia hilo, huku AMISOM ikiwa haijasema ikiwa wanajeshi wake waliuawa.
Wenyeji wa eneo hilo waliiambia BBC kuwa walisikia mlipuko mkubwa uliofuatiwa na ufyatulianaji mkali wa risasi.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP